Takriban watu wanane wameuawa katika mji mkuu wa Burundi,Bujumbura katika tukio lingine linalohusiana na maandamano ya kupinga hatua ya rais wa nchi hiyo
Rais Pierre Nkurunziza, alipoamua kuania muhula wa tatu wa uongozi.
Hii ni baada ya miili ya watu kupatikana mabarabarani na wakaazi wa vitongoji vya Bujumbura.
Mwandishi BBC mjini humo, anasema aliona maiti barabarani katika mitaa ya kaskazini mwa mji.
Alisema, baadhi yao wamepigwa risasi kichwani, na inaelekea walifungwa kwa kamba kabla ya kuuwawa.
Mapambano yalianza jana asubuhi, kwa risasi na maguruneti.
Afisa mkuu wa Polisi katika eneo hilo la Mutakura, Pierre Nkurikiye amewalaumu wahalifu kwa maafa hayo, lakini mitaa ya kaskazini mwa Bujumbura ni shina la upinzani dhidi ya Rais Pierre Nkurunziza.
Miili 6 ilipatikana katika kitongoji cha Cibitoke, ambacho kimekuwa shina la maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.
BBC.