Friday, August 07, 2015

UMEZALIWA DECEMBER 21 1994. HII INAKUHUSU! MENGI KUZAWADIA FEDHA VIJANA WALIOZALIWA TAREHE HIYO



UMEZALIWA DECEMBA 21 1994. HII INAKUHUSU! MENGI KUZAWADIA FEDHA VIJANA WALIOZALIWA TAREHE HIYO

Vijana wote wa Kitanzania waliozaliwa Desemba 21, 1994 watazawadiwa fedha taslimu na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, ikiwa ni zawadi yake kwa kutimiza umri huo ambao ni sawa na wa gazeti la Nipashe ambalo alilizindua jana likiwa na sura mpya. Dk. Mengi aliahidi kutoa zawadi hiyo kwa vijana wote wa Kitanzania waliozaliwa siku Nipashe ilipoanza kutoka ikiwa ni ishara ya kutambua mafanikio ya gazeti hilo.


Pia alisema zawadi kwa vijana hao ni sehemu na kielelezo cha kujumuika na Nipashe kwani sasa wamekua kiasi cha kuwa na umri unaokubalika kisheria kugombea ubunge.
"Unajua vijana waliozaliwa Desemba 21 mwaka 1994 siku nakala ya kwanza ya Nipashe inatoka, sasa wamekua na wanaweza kugombea ubunge," alisema Dk. Mengi.
Alisema kuwa kila kijana wa Kitanzania aliyezaliwa siku hiyo atazawadiwa Sh. 50,000, bila kujali idadi yao ilimradi tu athibitishe kwamba ana umri sawa na Nipashe, gazeti kongwe nchini.
Akizungumza katika hafla ya kuzindua Nipashe yenye muonekano mpya, Mkurugenzi Mtendaji wa The Guardian Limited (TGL), Richard Mgamba, alisema kuwa utaratibu wa jinsi ya kunufaika na zawadi hiyo utatolewa katika gazeti la Nipashe kuanzia wiki ijayo, na kila kijana wa Kitanzania atatakiwa kujaza vocha maalum itakayochapishwa katika gazeti hilo.
Kuanzia jana, Nipashe iliingia mtaani ikiwa na muonekano mpya ambao umezingatia mahitaji ya wasomaji na watangazaji ambao wamekuwa sehemu ya mafanikio ya gazeti hilo, ambalo limeshiriki kikamilifu kuripoti matukio mbambali ya kitaifa tangu mwaka 1994 hadi sasa. Nipashe iliandika kwa kina habari za matukio makubwa yaliyotokea nchini tangu Desemba 21, 1994.
Miongoni mwake ni chaguzi kuu nne zilizopita, 1995, 2000. 2005 na 2015; pia lilihabarisha umma juu ya janga la kuzama kwa meli ya Mv Bukoba mwaka 1996; ajali ya treni Dodoma 2002 na kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Oktoba mwaka 1999.
Mgamba alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, Nipashe itaripoti kwa weledi habari zote za uchaguzi, vyama na wagombea wake bila kuegemea upande wowote