Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya milipuko.
Takribani watu 22 wamejeruhiwa katika milipuko kadhaa ya mabomu iliyotokea katika ofisi za Usalama wa Taifa jijini Cairo, Misri mapema leo.
Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali ya Misri vimetangaza kuwa milipuko hiyo mitatu imetokea katika Wilaya ya Shubra al-Khaima.
Wizara ya Afya ya Misri imetangaza kuwa watu 29 wamejeruhiwa katika milipuko hiyo ingawa vyombo vya habari vya kujitegemea vimesema ni mapema kuweza kujua idadi ya watu waliouawa au kujeruhiwa katika milipuko hiyo.
Watu sita kati ya 29 waliojeruhiwa ni polisi, Wizara ya Mambo ya Ndani Misri imeeleza.
Misri imekuwa ikilengwa kwa mashambulizi yanayofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh ambayo kwa kawaida yanalenga taasisi za serikali hususani ofisi na idara za polisi na usalama wa taifa.