Watu 27 wameuawa na wengine wapatao 100 kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la bomu lililotokea muda mchache uliopita katika mji wa Uturuki wa Suruc.
Mji huo wa Suruc upo kwenye mpaka wa Uturuki na Syria.
Mlipuko huo ulitokea kwenye bustani ya kituo cha kitamaduni majira ya saa tatu.
Mamia ya vijana wanaripotiwa kufanya kazi kwenye kituo hicho.
Maafisa wanachunguza ikiwa mlipuko huo ulisababishwa na na bomu la kujitolea mhanga.
Mji wa Suruc, unapakana na mji wa Syria wa Kobane, ambao unawahifadhi wakimbizi wengi waliokimbia mapigano huko katika miezi ya hivi karibuni.
Mji wa Kobane umekua ni uwanja wa mapigano baina ya wanamgambo wa kutoka kundi la Islamic State (IS) na wapiganaji wa Kikurdi tangu mwezi wa Septemba mwaka jana , pale IS walipouteka mji huo , na kuwalazimisha wengi wa wakazi wa mji huo kukimbilia ndani ya Uturuki.