Mamilioni wa raia nchini Ugiriki wanapiga kura ya maamuzi kuhusu iwapo watakubali ama kukataa masharti yaliowekwa na wakopeshaji ili kulipa deni wanalodaiwa.
Akipiga kura,waziri mkuu Alexis Tsipras amesema kuwa hakuna anayeweza kupuuza uamuzi wa raia.
Serikali yake ya mrengo wa kushoto imewashauri wapiga kura kuyakataa mapendekezo yaliyotolewa na wakopeshaji wake.
Lakini viongozi wa Ulaya wameonya kuwa kura ya 'LA' itasababisa Ugiriki kuondoka kwenye nchi zinazotumia sarafu ya Yuro.
Kura ya maoni inaonyesha kuwa huenda matokeo yakakaribiana sana.
Benki nchini Ugiriki zimefunwa tangu wiki iliyopita huku uchumi ukiathirika pakubwa
BBC.