Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, amedhihirisha zaidi, kwamba anataka wanajeshi wa Uingereza wawashambulie wapiganaji wa Islamic State nchini Syria.
Aliiambia televisheni ya Marekani, London, kwamba amejitolea kushirikiana na Marekani, kuiangamiza IS nchini Iraq na Syria.
Wanajeshi wa Uingereza tayari wanashiriki katika mashambulio dhidi ya IS nchini Iraq.
Lakini alikiri kuwa anahitaji kuungwa mkono na bunge.
Miaka miwili iliyopita, wabunge walipinga kuingia Syria kijeshi.
Juma lilopita, ilibainika kuwa marubani wa Uingereza wanarusha ndege zinazoshambulia IS nchini Syria, lakini marubani hao wako chini ya uongozi wa jeshi la nchi nyengine.
BBC.