Friday, May 08, 2015

UINGEREZA YAPATA MBUNGE MCHINA



UINGEREZA YAPATA MBUNGE MCHINA
alan_mak

Mbunge Allan Mak

 

 

Alan Mak amekuwa ni Mwingereza wa kwanza mwenye asili ya China kuwa Mbunge katika Bunge jipya  la Uingereza. Pamoja na kuwa na asili ya China ameshasema kuwa uasili wake hautamfanya awe anawapendelea Wachina wenzie. Amesema swala ukabila analiona kama ni tatizo. Mbunge huyu mwenye umri wa miaka 31 alimshinda mpinzani wake John Perry kwa kupata asilimia 51 ya kura zote na kuweza kupata Ubunge kupitia chama cha Conservative.

Mak atakuwa Mbunge wa mji wa Havant. Mak alizaliwa York, wazazi wake walikimbia kwao enzi za utawala wa Kikomunisti wa MaoTse Tung kwenye miaka ya 60, na kutua Uingereza.

Katika website yake Mak alisema anaipenda Conservative kwa vile familia yake inajua ugumu wa maisha bila Conservative kuweko madarakani. Pamoja ya kuwa kuna Wachina 426,000 Uingereza kadri ya sensa ya 2011, Mak hana mpango kabisa wa jina lake kutajwa kwa sifa kama ilivyokuwa kwa Bernie Grant, Paul Boeteng na Diane Abbot Wabunge wa kwanza weusi waliochaguliwa 1987, au Chris Smith Mbunge wa kwanza kujitangaza hadharani kuwa yeye ni shoga, ambaye aliingia Bungeni 1983. Mak amesema yeye anasimama kwa ajili ya watu wake wa Havant na nchi yake ya Uingereza