Friday, May 08, 2015

VIONGOZI WA UPINZANI UINGEREZA WAJIUZURU BAADA YA VYAMA VYAO KUSHINDWA UCHAGUZI


VIONGOZI WA UPINZANI UINGEREZA WAJIUZURU BAADA YA VYAMA VYAO KUSHINDWA UCHAGUZI
index

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron

 

Katika ushindi usio na ubishi, David Cameron amerudi kwenye uongozi wa Uingereza na kurudi tena kutumia ofisi ya No10 Downing Street, baada ya chama chake cha Conservartives kushinda kwa kile ambacho Cameron amekiita 'the sweetest victory of all' mpaka sasa inaonekana wazi kuwa Conservartives watashinda viti 331 ambavyo vitawapa nguvu ya kuongoza katika House of Commons.Kimsingi kuwa na uongozi wa chama kimoja.

Wakati tayari majimbo 638 kati ya majimbo 650 yametangazwa, Conservatives walikuwa wamepoteza majimbo yao ya awali 11, lakini wamepata majimbo mapya 32. Ila kulikuweko na jambo jipya katika uchaguzi huu chama cha Scottish National Party (NSP) cha Scotland kimepata nguvu sana katika uchaguzi huu kwa kupata wabunge wengi zaidi kuliko ambavyo imekuwa awali.Mpaka sasa hali ni kama ifuatavyo;

Conservatives  viti 327 -50%

Labour Party viti 232 -36%

SNP viti 56 -9%

Liberal Democrats viti 8  -1%

UKip kiti 1 0%

Katika historia ya uchaguzi wa ni mara ya kwanza toka mwaka 1963 ambacho cham kilichoko madaraka kuongeza ushindi mkubwa kiasi kama uchaguzi huu

ed_miliband

Ed Miliband aliyekuwa kiongozi wa Labour Party

Kiongozi wa Labour Party amejiuzuru uongozi wa chama hicho baada ya chama hicho kupata hasara ya kunyang'anywa viti kadhaa katika uchaguzi huu. Chama cha SNP na Conservative vimechukua viti kadhaa vilivyokuwa vya chama hicho. Ed Milliband aliyejiunga na Labour Party akiwa na miaka 17 amesema wakati anajiunga hakuota ndoto kuwa ataweza kuja kuwa kiongozi wa chama hicho, kwa vile ameshindwa kukipa ushindi cham chake, alisema anawaachia wengine nao waone namna ya kukijenga ili kiweze kushika uongozi katika muhula ujao. Kiongozi huyo alisema Naibu wake Harriet Harman atashika uongozi wa muda baada ya yeye kuachia ngazi .

election_farageb

Aliyekuwa kiongozi wa Lib Dem Bwana Glegg

 

Wakati huo huo  Bwan Clegg kiongozi wa Liberal Democrats nae alisema anajiuzuru japo kuwa amepata kiti cha Ubunge na ataendelea nacho, Kiongozi wa UK Independence Party Nigel Farage, ambae amekosa hata jimbo, nae ameachia ngazi ya uongozi katika chama chake