Saturday, April 04, 2015

Wafanya biashara wasitisha mgomo wao mjini Songea.

[image]
Wakati mgomo wa wafanyabiashara wa kutofungua maduka ukiendelea mjini
Songea mkoani Ruvuma mgomo wa waendesha Daladala uliodumu kwa siku
nzima jana umesitishwa.
Mwenyekiti wa wasafirishaji wa mkoa wa Ruvuma Bw.Golden Sanga amesema
kuwa wameamua kusitisha mgomo wa Daladala ili kutoa nafasi ya Viongozi
kusikiliza malalamiko ya wafanyabiashara huku mgomo wa kutofungua
maduka ukiendelea.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Ruvuma Bw.Isaya
Mbilinyi amesema kuwa madai yao yasiposikilizwa ya kutatuliwa utata
wa mashine za EFDS,ongezeko la kodi kwa asilimia mia moja na kuachiwa
kwa dhamana mwenyekiti wao wa taifa Bw.Johnson Minja mgomo huo utakuwa
endelevu.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Mwambungu anawasihi
wafanyabiashara kusitisha mgomo wao kwa kuwa kuendelea kugoma ni
kuwaumiza wasio na hatia bila sababu ya msingi.

Wakati hayo ya kijiri huko tayari Mwenyekiti wa wafanya biashara
Bwana.Johnson Minja amepewa Dhamana na mahakama Hakimu Mkazi Mkoa wa
Dodoma.