Tuesday, April 14, 2015

FEDHEHA KUBWA MUME WA MTU AKUTWA NA CHANGUDOA AKIVAA SURUALI









Wakihamaki baada ya kukurupushwa.

Tumenasa tukio la aina yake ambapo mwanaume aliyejitambulisha kuwa ni mume wa mtu amekutwa na mwanamke changudoa akivaa suruali baada ya kuvunja amri ya sita ya Mungu kwenye eneo la biashara ya mamantilie!
Tukio hilo la aina yake lilinaswa kwenye uchochoro mmoja, maeneo ya Mwenge, Dar, majira ya saa 9:00 usiku ambapo wahusika hao ambao hawakutaka kutaja majina walikutwa wakiwa wanavunja amri ya sita kabla ya kushtuliwa na mwanga wa kamera yetu.
Wakiwa wanakatiza kwenye uchochoro huo, tulisikia miguno ya kimahaba ambapo ilibidi kutulia kidogo kujua kunani kinachoendelea mahali hapo.
Waliposogelea waliwashuhudia wawili hao wakiwa wamevua nguo ambapo mwanamke alikuwa ametandika khanga chini bila kujali mtu anaweza kukatiza na kushuhudia sinema yao ya ngono.
Dada huyo akivaa baada ya fumanizi hilo.
Mara baada ya kuwafotoa picha kadhaa, wawili hao walishtuka huku mwanamke akivaa nguo harakaharaka kabla ya mwenzake naye kuvaa kisha wakataka kuanzisha timbwili.

"Huyu dada yeye hana shida sana kwani siyo mke wa mtu. Tatizo lipo upande wangu maana mkinitoa itakuwa fedheha kwa mke na watoto wangu," alijitetea jamaa huyo.
Baada ya aibu hiyo, wawili hao waliondoka mahali hapo na kutimkia kusikojulikana.