Wednesday, April 08, 2015

Dr Shein amesema serikali zote mbili nchini zimekubaliana kutunga sheria za kuwaenzi waasisi wa Tanzania.





Dr Shein amesema serikali zote mbili nchini zimekubaliana kutunga sheria za kuwaenzi waasisi wa Tanzania.
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohamed Sheiin amesema seriklai zote mbili nchini zimekubaliana na kutunga sheria maalum ya kuwaenzi waasisi wa Tanzania na bodi tayari imeundwa huku akiwataka vijana nchini na viongozi kuiga na kufuata kwa vitendo utendaji na uendeshaji wa uongozi wa marehemu Abeid Amani Karume.
Dr Shein ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar ametoachangamoto hiyo hapa Zanzibar baada ya kuyapokea matembezi ya vijana waliotembea kutoka Mwera wilaya ya kati hadi ofisi kuu ya CCM kumeunzi rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume ambapo alisema marehemu Karume alikuwa kiongzoi wa vitendo hivyo kuwataka vijana kumuenzi muasisi huyo wa mapinduzi.
 
Katika hatua nyingine Dr Shein amesema tayari serikali ya jamhurri ya mungano imepitisha sheria na imeunda bodi ambayo imeshanza kazi ya kuwaenzi waasisi wa Tanzania ikiwana na lengo la kuhakikisha historia ya viongozi hao wawili inabakia na inatunzwa.
 
Mapema naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali alisema CCM itakuwa vyema vijana hao kutekeleza yale ambayo wanayashauri huku  vijana katika risala yao wameitaka serikali kujenga nyumba  maalum  eneo alipozaliwa marehemu Abeid Amani Karume ambayo itakuwa na hadhi na kumbukumbu za rais huyo.
 
 
Matembezi ya vijana hao yalianzia Mwera kiongoni wilaya ya magharibi sehemu ambayo ndipo alipozaliwa marehemu Abeid Amani Karume rais wa kwanza wazanzibar na vijana hao walitembea kwa miguu kutoka hapo mpaka ofisi kuu ya CCM wilaya ya mjini.