Wednesday, April 08, 2015

Rais mstaafu Mhe.Benjamini Mkapa amezitaka nchi za Afrika kulinda rasilimali.



Rais mstaafu Mhe.Benjamini Mkapa amezitaka nchi za Afrika kulinda rasilimali.
Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Mhe.Benjamini Mkapa amesema nchi za afrika zinaweza kuingia katika vita vya ndani kutokana na mikataba ambayo mataifa makubwa yanayataka kuingia kwa madhumuni ya kunusuru hali zao za maisha katika mataifa yao.
Akizungumza na wanachuo cha ulinzi cha taifa, kuhusu tathimni yake ya hali ya dunia na uwezekano wa kutokea vita kwa nchi moja moja ametaka baadhi ya mikataba iliyoingiwa katika nchi za afrika kurudi katika mazungumzo na ishirikishe zaidi wananchi wa sekta husika ambapo amezitaka serikali za afrika kulinda maliasili na kuhakikisha mikataba wanayotiliana saini na mataifa makubwa inalinda haki na maslahi ya wananchi.
 
Rais mstaafu Benjamni Mkapa ametaka umoja wa mataifa ufumuliwe na kuundwa upya hususani taasisi yake ya baraza la usalama kutokana na mabadiliko yaliojitokeza duniani na kuibuka kwa baadhi ya mataifa ambayo yamekuwa makubwa na kuwa na nguvu za kiuchmi na silaha na kustahili kuwa wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.
 
Aidha amepinga uwezekano wa kutokea vita kuu ya tatu ya dunia kutokana na maendeleo ya yaliyojitokeza kisalaha katika baadhi ya nchni, na kusisitiza vitavinavyoweza kutokea ni kuokana na uongozi mbaya, tamaa za baadhi ya nchi kutaka kupanua maeneo ya nchi zao pamoja na njaa.