Wednesday, April 08, 2015

IS yazidi kusaka wafuasi



IS yazidi kusaka wafuasi
Is na kiu ya kuongeza wafuasi zaidi
Binti mmoja mwenye asili ya Afrika Kusini ameshushwa kwenye ndege mjini Cape Town baada ya kushukiwa kuwa na mpango wa kutaka kwenda kujiunga na kundi la wanamgambo wa Islamic State (IS), waziri wa mambo ya ndani wan chi hiyo ameyasema hayo.
Familia ya binti huyo ilichukua jukumu la kuwasiliana na polisi,baada ya kutoweka nyumbani kwao mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mapema mwaka huu mnamo mwezi wa pili, taarifa zilienea katika mitandao ya kijamii kwamba kuna mtu kutoka Afrika Kusini amejiunga na kundi la IS nchini Syria,na alikuwa akijaribu kukusanaya vijana wengine kutoka katika nchi hiyo wajiunge na kundi hilo kupitia mitandao ya kijamii,na hiyo ni kesi ya kwanza kuripotiwa ,kwa mtu kutoka nchini humo kujiunga na kundi hilo.
Binti huyo anayeshukiwa kula njama za kutaka kujiunga na kundi hilo,ana umri wa miaka kumi na mitano tu,na alikuwa amekata tiketi ya shirika la ndege la British Airways ,lakini jaribio lake liligonga mwamba baada ya polisi kumfuatilia,kumshusha kwenye ndege na kumkabithi kwa wazazi wake waliokuwa wakimwemweseka tabasamu la furaha baada ya kumpata tena binti yao;wazo lake la kutaka kujiunga na kikundi hicho lilipingwa vikali na jamaa yake.
Kwa muda mrefu binti huyo alikuwa akionekana kushughulika zaidi na vifaa vya kiteknolojia,mitandao ya kijamii,akiwasiliana na watu ambao ni wageni machoni pa jamaa yake,lakini pia alikuwa ni mwenye kujisomea maandishi yanayomuelekeza kuwa na tamaa ya kujiunga na kundi hilo la kigaidi.
Maofisa wa Marekani wanaamini kwamba zaidi ya elfu ishirini kutoka nchi zaidi ya mia moja wameelekea nchini Syria na Iraq ,mahali ambako IS wametandaza himaya yao.
Lakini pia maofisa kutoka nchini Uingereza wameongeza kwamba raia wao wapatao mia sita wamejiunga na kundi hilo.
Wimbi la vijana wengi duniani hukimbilia kujiunga na makundi ya kigaidi
IS wamefanikiwa kukita utawala wao katika bara la Afrika, wakiwa na makundi ya askari wao katika nchi za Nigeria na Libya na wamekuwa wakikiri kuhamashisha ulipuaji majengo kwa jina lao.
Manmo mwezi February, gazeti la kila wiki la nchini Afrika kusini limekaririwa likidai kwamba mtu mmoja mwenye asili ya Afrika Kusini anayejiita Abu Hurayra al-Afriki amesha jiunga na kundi hilo la IS nchini Syria.
Na amekwisha fungua kurasa za mtandao wa Tumblr na Twitter yeye akiwa kama mshauri wa namna ya kuwa mjitoa muhanga na namna ya kufanya. Japokuwa kurasa hizo zimesitishwa na wana usalama wa mtandao.