Thursday, April 16, 2015

BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.



BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.
unnamed
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkaribisha  Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing  alipomtembelea  ofisini kwake  leo jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo  ya kuimarisha  ushirikiano kati ya Tanzania na China katika masuala ya uendelezaji wa Ardhi na Mipango miji.


LUK1Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia)  akimweleza  Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing  (kushoto) namna Wizara yake  inavyoendelea  kuimarisha  shughuli za Mipango Miji ,Usimamizi na Matumizi endelevu ya Ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.LUK2Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia)  akiwa katika mazungumzo na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania uliomtembelea leo Ofisini kwake ukiongozwa na Balozi Lu Youqing  (kushoto)  kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya China na Tanzania katika kuimarisha  shughuli za Mipango Miji ,Usimamizi wa Matumizi endelevu ya Ardhi .
LUK3Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Alphayo Kidata  (kushoto) akifurahia jambo wakati akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania ulioitembelea  Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuendeleza  ushirikiano kati ya China na Tanzania katika  Matumizi endelevu ya Ardhi