Thursday, April 02, 2015

ALIYEWAUA WAINGEREZA WAWILI KUNYONGWA



ALIYEWAUA WAINGEREZA WAWILI KUNYONGWA


MAHAKAMA nchini Malaysia imemkuta na hatia ya mauaji Zulkipli Abdullah kwa tuhuma za mauaji ya wanafunzi wawili wa udaktari waliokuwa raia wa Uingereza.



Kwa mujibu wa Shirika la Habari la DW, mauaji hayo yalifanyika mwezi Augosti mwaka jana katika kisiwa cha Borneo.

Jaji wa mahakama hiyo amesema kuwa mahakama imeridhishwa na ushahidi dhidi ya mshtakiwa na kuona anastahili adhabu.

Zulkipli Abdullah anadaiwa kuwaua Neil Dalton na Aidan Brunger ambapo adhabu iliyotolewa na mahakama hiyo ni kunyongwa hadi kufa.