Friday, April 10, 2015

AKAUNTI 86 ZA WATU BINAFSI ZAFUTWA KENYA



AKAUNTI 86 ZA WATU BINAFSI ZAFUTWA KENYA
Waziri mstaafu wa mambo ya ndani wa Kenya Joseph Nkaissery, ameithibitishia BBC kwamba serikali ya Kenya imesitisha matumizi ya akaunti za watu binafsi wapatao themanini na sita wanaohusishwa na ufadhili wa kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini humo.


Akaunti za watu hao ambao zimesitishwa ni baadhi ya watu waliokuwa katika orodha ya serikali ya Kenya ambao walikuwa wakifuatiliwa mienendo yao.Kufuatia hali hiyo nayo makampuni kumi na tatu ya ubadilishaji na usafirishaji fedha nayo yamefungwa.
Serikali ya Kenya imetoa ushari kwa wateja wa mabenki wa madhehebu ya dini ya Kiislamu kutumia akaunti za benki za Sharia ambazo zimethibitishwa na benki kuu ya Kenya.
Msemaji wa Muungano wa Wanaosafirisha fedha kwa njia ambayo inajulikana kama Hawala ambao nao pia wamezuiwa Abdi Ali anasema wako makini na uamuzi huo na kwamba tayari wamewaagiza wanasheria wao kushughulikia hali hiyo.
Kujua zaidi juu ya hatua hiyo Regina Mziwanda amezungumza na Mchambuzi wa Masuala ya Somalia Mohamed Abdillahi, Juu ya taarifa za serikali ya Kenya kufunga akaunti nane za watu wanaoshukiwa kuwa wafadhili wa Al Shabab,kuna maana gani wakati huu.?
BBC.