Monday, February 02, 2015

Watu wawili wafa papo hapo kwa kugongwa na gari wilayani Ngara mkoani Kagera



Watu wawili wafa papo hapo kwa kugongwa na gari wilayani Ngara mkoani Kagera
Watu wawili wamekufa papo hapo baada ya kugongwa na  gari dogo lenye namba za usajili  T 346 DAA katika eneo la Lemela ,katika barabara ya Kabanga-Ngara wilayani Ngara mkoani Kagera.



Pichani ni miili ya watu wawili waliofariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari  dogo aina ya Saloon ,majina ya marehemu hao hayakupatikana mara moja na kwa mujibu wa mashuhuda wamesema kuwa  chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.







Pichani ni gari hilo dogo aina ya Saloon likiwa  limeharibika vibaya baada ya kugonga watu wawili na kufa papo hapo eneo la Lemela mjini Ngara.

Askari wa usalama Barabarani akipatia ushahidi wa baskeli iliyoharibika vibaya baada ya kugongwa na gari dogo aina ya Saloon lenye namba za usajili T 346 DAA katika eneo la tukio na kuvipeleka kituo cha Polisi.


,chini ni Baiskeli aliyokuwa ikitumiwa na Marehemu hao ikiwa imeharibika vibaya