WAKAZI wa eneo la Kawe-Bondeni jijini Dar es Salaam wameamua kukaa katikati ya barabara eneo hilo wakiishinikiza serikali kuwawekewa matuta wakidai kuchoshwa na ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikiondoa uhai wa wapendwa wao wakiwemo wanafunzi.
Wananchi hao wamefikia uamuzi huo leo baada ya jana mtu mwingine kugongwa eneo hilo na kupoteza maisha.