Wednesday, February 25, 2015

Waethiopia 13 wakamatwa wakisafirishwa Morogoro



Waethiopia 13 wakamatwa wakisafirishwa Morogoro
Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro  limewakamata  wahamiaji haramu 13  kutoka nchini  Ethiopia wakiwa kwenye gari ndogo aina Prado  katika kijiji cha Lusanga  Turiani  wilayani Mvomero wakijiandaa kwenda Afrika kusini kupitia mkoani Mbeya .

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro ACP leonard Paul  akizungumzia  tukio hilo amesema waethiopia hao walitokea nchini Kenya na kupita Handeni na kuingia wilayani Mvomero na walikuwa wakijiendaa kwenda Mbeya kabla ya kwenda nchini Afrika Kusini kutafuta hifadhi.
  
Jeshi hilo pia linamshikilia dereva wa gari hiyo na wanafanya mawasilinao na idara ya uhamiaji na baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.
  
Naye dereva wa gari ndogo aina ya Prado  Musa Edmund  akiongea  huku akionekana kuficha sura yake  anayeshikiliwa kwa kusafirisha waethiopia hao amesema alimpeleka boss wake Arusha njiani wakati anarudi  alikutana na waethiopia hao  mbapo waliomba awasafirishe kwa  makubalinao kuwa  atalipwa shilingi milioni moja hadi kuwafikisha mkoani Mbeya ambapo alilipwa nusu ya gharama hizo kwa makubalino malipo mengine yangefanyika baada kuwafikisha mkoani Mbeya