Serikali ya Tanzania imedokeza kuna uwezekano wa kuweka historia kwa Watanzania waishio nje kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.
Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda akizungumza na wabunge wa nchi hiyo Bungeni Dodoma, katikati mwa Tanzania, amesema Tume ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya uchaguzi Zanzibar(ZEC),tayari wameanza kufanyia kazi mipango ya kuwezesha Watanzania waishio nje waweze kushiriki zoezi la kupiga kura.
"Watanzania walio nje wana haki kushiriki katika zoezi hili na tuna nia ya kuona hilo linafanyika."alieleza Waziri Pinda
Hata hivyo imesemekana kuna changamoto za kiufundi ambazo amesema anaamini tume ya uchaguzi NEC na ZEC zitashughulikia