Saturday, February 07, 2015

Mamia ya wakazi wa Kigamboni wanaotumia usafiri wa MV Kigamboni wamekwama kwa zaidi ya saa mbili



Mamia ya wakazi wa Kigamboni wanaotumia usafiri wa MV Kigamboni wamekwama kwa zaidi ya saa mbili

Mamia ya wakazi wa Kigamboni ambao wanatumia usafiri wa MV Kigamboni wamekwama kwa zaidi ya saa mbili huku wengine wakilazimika kutumia viboti vidogo kwa ajili ya kuvuka upande wa pili ili kuwahi katika shughuli zao kufuatia kutokuwepo kwa kivuko hicho na hivyo kutumika kwa kivuko kimoja tuu.

Wakizunguza kivukoni hapo baadhi ya waathirika wa tukio hilo wamesema wamelazikia kugombea kivuko kimoja kilichokuwa kikifanya kazi huku wengine hasa wanafunzi wanaosoma chuo cha usimamizi wa fedha IFM ambao wengi wao wanaishi Kigamboni kujikuta wanachelewa kwenye mitihani.
 
Kutokana na hali hiyo ya kivuko kujirudia rudia kuharika baadhi ya watumiaji wa kivuko hicho wameshauri ni bora huduma za vivuko hizo zikabinafishshwa ili kupata mwekezaji atakayeweza kuviendesha vivuko hivyo kwa uhakika kabla madhara zaidi hayajatokea.
 
Tuliutafuta uongozi wa wakala wa ufundi na umeme Temesa kuzungumzia hali hiyo ambapo afisa mtendaji mkuu Bi Marcellin  Magesa amesema kivuko hicho kilikuwa katika matengenezo ya kawaida na kilipokuwa kilifanyiwa matengenezo kilipoteza mwelekeo injini zikazima baada ya kuingia takataka.