Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Juma Bwire akiwaonesha waandishi wa habari risasi zilizokamatwa katika operesheni maalumu iliyofanikiwa kumtia nguvuni kijana huyo Wolfram Msemwa anayedaiwa amekuwa na mtandao na baadhi ya waharifu kutoka nchi jirani na Tanzania kwa upande wa Magharibi.
Jumla ya risasi 356 za SMG zilizokamatwa askari Polisi kwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Wolfram Msemwa(32) huko katika mtaa wa Kazehill kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora.