Tuesday, January 06, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI



WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega kabla ya kuanza ziara katika wilaya hiyo ili kujionea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini pamoja na kuzungumza na wananchi.
Mkazi wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi (hawapo pichani) mara Waziri alipofanya mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho ili kusikiliza kero zao.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwenye mkutano na wananchi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma ( wa mwisho kushoto) ya kuitaka Tanesco kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme vijijini.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo katika mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Bushigwamala wilayani Busega (hawapo pichani).
Sehemu ya umati wa wananchi wa kata ya Kalemala wilayani Busega waliojitokeza kwenye mkutano na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakifuatilia kwa makini hotuba yake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo wilayani Busega Bw. Steve Thomson (kushoto).
Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega (hawapo pichani).
Mkazi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega ambaye jina lake halikupatikana mara moja akitoa hoja yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto waliosimama mbele) mara Waziri alipofanya ziara katika kijiji hicho na kusikiliza kero za wananchi.
Diwani wa Kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega Vumi Magoti akielezea kero za umeme katika kata yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto), viongozi na wananchi (hawapo pichani).