Monday, January 05, 2015

Raia wa Syria wapewa masharti Lebanon


Raia wa Syria wapewa masharti Lebanon
Lebanon imepokea Wakimbizi zaidi ya
Wakimbizi milioni moja kutoka nchini Syria 


Masharti mapya yamewekwa na mamlaka ya Lebanon kwa Raia wa Syria wanaoingia nchini humo , wakati huu ambapo nchi hiyo inapokea
Wakimbizi wengi.

Kwa mara ya kwanza, Raia wa Syria watalazimika kuwa na vielelezo vinavyoeleza kwa nini wanataka
kuvuka mpaka na kuingia nchini Lebanon.

Masharti haya mapya yanaanza kutumika siku ya jumatatu.Awali kusafiri kati ya nchi hizo mbili kwa kiasi kikubwa hakukuwa na kikwazo lakini sasa
Raia wa Syria lazima wawe na Viza.
Hatua hii inaelezwa kulenga kudhibiti idadi kubwa ya Wakimbizi wanaoingia nchini Lebanon, ambapo kwa sasa Lebanon ina wakimbizi zaidi ya milioni
moja.

Hatua hii ya sasa haijulikani italeta athari gani kwa Raia wengi wa Syria walio nchini Lebanon ambao
hawajajiandikisha kuwa wakimbizi.

Kabla ya sasa, Raia wa Syria waliweza kukaa nchini Lebanon mpaka miezi sita, lakini sasa raia wa nchi hiyo watalazimika kutimiza vigezo kadhaa
ili kupatiwa Viza mpakani.