Thursday, January 08, 2015

MWIGULU NCHEMBA AMETIMIZA MIAKA 40,ATUMIA SIKU YAKE KUCHANGIA DAMU,KUSALIMIA WATOTO YATIMA NA KUJULIA HALI WODI YA AKINAMAMA MWANANYAMALA



MWIGULU NCHEMBA AMETIMIZA MIAKA 40,ATUMIA SIKU YAKE KUCHANGIA DAMU,KUSALIMIA WATOTO YATIMA NA KUJULIA HALI WODI YA AKINAMAMA MWANANYAMALA
Mh:Mwigulu Nchemba hii leo ametimiza miaka 40 ya Kuzaliwa kwake.Mwigulu Nchemba akiwasili Hospitali ya Mwananyamala kwaajili ya Kutembelea na kusalimia Wodi ya wazazi kama sehemu yake ya Kusherekea siku ya Kuzaliwa(Miaka 40).Mwigulu Nchemba akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Mwananyamala hii leo tar.07.01.2015.Mh:Mwigulu Nchemba akimsalimia mtoto aliyepatwa na tatizo la kuungua moto.Mh:Mwigulu akisikiliza kwa
makini mahitaji ya wodi ya akinamama kutoka kwa Mganga mkuu Hospitali ya Mwananyamala.Mwigulu Nchemba akisaidia kubeba mtoto wakati alipotembelea \hospitali ya Mwananyamala hii leo kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.Mwigulu Nchemba akizungumza na Bi.Saida ambaye ni Mwenyekiti wa kituo cha watoto yatima cha CHAWAKAMA.Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba Bi.Neema Ngure akisaidia kubeba mtoto Yatima kwenye kituo cha watoto yatima Sinza hii leo.Baadhi ya watoto yatima wakimsikiliza Mwigulu Nchemba.Mwigulu Nchemba akiwapatia watoto yatima zawadi kwa yeye kutimiza miaka 40,Mwigulu Nchemba amefanya hivyo hii leo kwenye kituo cha watoto yatima CHAWAKAMA Sinza Jijini Dsm wakati alipotembelea kwaajili ya kuwajulia hali.Katika hatua nyingine Mh:Mwigulu Nchemba ametumia siku yake ya kuzaliwa (Miaka 40) kuchangia Damu salama kwaajili ya kusaidia watanzania wanaopatwa na Matatatizo ya kuhitaji damu.Mwigulu amefanya tukio hilo hii leo Jijini Dsm kwenye kituo kikuu cha kuchangia Damu IlalaMh:Mwigulu Nchemba akioneshwa sehemu ya kuhifadhia damu na namna inavyohifadhiwa.Mh:Mwigulu Nchemba na Mke wake wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Kitengo cha Damu salama mara baada ya kuchangia Damu/

HONGERA SANA HON;MWIGULU NCHEMBA KWA KUTIMIZA MIAKA 40