Sunday, January 04, 2015

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AZINDUA WA BARABARA YA MKAPA AWAMU YA PILI


MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AZINDUA WA BARABARA YA MKAPA AWAMU YA PILI
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Zanzibar Seif Ali Iddi akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Barabara ya Amani- Mtoni kwa awamu ya pili ya ujenzi wake katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. (kushoto alievaa kofia ya pama) Katibu Mkuu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Malik Akili.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuzindua Barabara ya Mkapa iliopo Amani-Mtoni ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar (kushoto) Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji.
Baandhi ya wananchi na Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Barabara ya Mkapa iliopo Amani-Mtoni Mjini Zanzibar.
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji akitoa nasaha fupi na kumkaribisha Balozi Seif Ali Iddi kutoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Mkapa iliopo Amani-Mtoni Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akihutubia katika Sherehe ya uzinduzi wa Barabara ya Amani-Mtoni ikiwa ni miongoni wa shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Picha ya Barabara ya Amani-Mtoni iliyozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.