Na Abou Shatry DMV
Kama vile matangazo ya hali ya hewa yalivyo tolewa mwazoni mwa wiki hii na National Weather Service, katika maeneo mbali mbali ya hapa DMV kwamba hali ya hewa itazidi kuwa baridi na kutegemea kuanguka theluji ya inches mbili hadi tatu katika maeneo mbali mbali hapa DMV
Theluji hiyo iliotarajiwa kuanguka mapema mapema mida asubuhi 6: AM ya leo Jumanne Jan,6 na kutegemea kusimama kuanguka mida ya 11:AM ya Saa tano mchana .
Aidha maeneo mbali mbali ya barabara kuu yameonekana kufanyiwa usafi mapema na magari ya usafishaji kumwagiliaji chumvi maalumu ambazo hupunguza mitelezo inayotokea mara kwa mara wakati theluji hizo zinapotokea kila ifikapo msimu wa baridi.
Pia tunapenda kutoa tahadhari kwa Madereva wa magari kuwa makini na theluji ambayo husababisha ajali za barabarani na haswa mnapokuwa katika barabara kuu za Highway na njia za ndani, kwa maana hadi sasa mitelezo na mafoleni baadhi ya maneno mbali mbali yameshaanza kujitokeza katika baadhi ya mabarabara Ndani ya DMV kwa hiyo tunawaomba waTanzania wote wanaoishi maeneo yaliokubwa na theluji hiyo kuwa makini wakati unapoendesha gari lako.