Meneja Mkuu wa na Hoteli ya Giraffe Ocean View, Evelyn Mwasela akizungumza baada ya kukabidhi zawadi ya mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia kwa ajili ya Sikukuu ya Krimasi kwa watoto wa Kituo cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyofanyika hoteli hapo ilihusisha pia chakula cha mchana.
Watoto wa Kituo cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, Dar es Salaam, wakijihudumiwa chakula cha mchana juzi kilichoandaliwa na Hoteli ya Giraffe Ocean View iliyopo jijini ambapo pia walipewa zawadi ya mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia kama zawadi ya Sikukuu ya Krismasi.
Mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, Cecilia Ismail (kulia), akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake, baada ya kukabidhiwa mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia kama zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Hoteli ya Giraffe Ocean View, Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyoambatana na chakula cha mchana ilifana asana.
Watoto wanaolelewa katika Kitu cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, wakiwasili katika eneo la Hoteli ya Giraffe Ocean View, Dar es Salaam juzi baada ya kualikwa kwa ajili ya kupewa zawadi ya Sikukuu ya Krismasi pamoja na chakula cha mchana.
Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, wakicheza muziki katika ukumbi wa Hoteli ya Giraffe Ocean View, Dar es Salaam juzi baada ya kualikwa kwa ajili ya kupewa zawadi ya Sikukuu ya Krismasi pamoja na chakula cha mchana
Meneja Mkuu wa na Hoteli ya Giraffe Ocean View, Evelyn Mwasela (kushoto), akizungumza baada ya kukabidhi zawadi ya mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia kwa ajili ya Sikukuu ya Krimasi kwa watoto wa Kituo cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, Dar es Salaam.
Danielle Taboada raia wa Uswisi (katika), akimsaidia mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa na Hoteli ya Giraffe Ocean View, jijini Dar es Salaam. Hoteli hiyo iliwaalika watoto hao kupata chakula cha mchana pamoja na kuwapa mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia kama zawadi ya Sikukuu ya Krismasi.