Benki ya NMB kwa kushirikiana na Azam FC jana wamezindua rasmi kadi za wanachama wa klabu hiyo amabazo zitawawezesha kupata huduma za kibenki za NMB zilizotapakaa nchi nzima.
Naibu Waziri wa Habari ,Vijana ,utamaduni na michezo Mhe. Juma Nkamia ndie alikuwa mgeni rasmi katika hafla hii. Pia aliwataka wanachama kuiunga mkono timu hiyo kwa matokeo yoyote.
"Mashabiki najua kazi zenu ni mbili kushangilia na kuzomea timu pinzani hivyo nawataka muwe na mapenzi ya dhati na timu yenu kwani naamini kuizomea timu ni ishara ya kwamba kuna tatizo mahali na kuishangilia timu ni kuashiria mambo yapo safi" aslisema.
Kwa upande wa NMB, Afisa Mkuu wa Fedha Bw. Barnabas Waziri alisema kuwa NMB itaendelea kushirikiana na AZAM kukuza mpira hapa nchini na vile vile kuhakikisha kwamba mashabiki wa mpira wanapata nafasi ya kupata huduma za kibenki kwa rahisi na karibu zaidi.
Naibu Waziri wa Habari ,Vijana ,utamaduni na michezo Mhe. Juma Nkamia akiongea na wanachama wa AFC pamaoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kati hii ya uanachama.
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hii katika viwanja vya Azam jana.
Mmoja wa wanachama akionyesha kadi yake aliyokabidhiwa kama mwanachama wa Azam FC.