Serikali imelifungia                shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili kutokana na                sababu mbalimbali na ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea,                ikiwemo udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka kwenye                shidano hilo.
        Maamuzi hayo                yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza                hilo Godfrey Mngereza amesema maamuzi                hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao cha tathmini ambapo                Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za msingi                za wadau na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa                shindano hilo.
        "Baada ya kupitia                  maelezo yote na taarifa ya tathmini ya shindano hilo ni                  vyema tulisimamishe kwa muda ili mwandaaji ajipange                  upya, atakaporejea arejee kwa nguvu na kuandaa shindano                  lenye hadhi kubwa kuliko ilivyo hivi sasa'' alisema Mngereza.
        Shindano hilo                limekumbwa na kashfa mbalimbali tangu mwaka 2006 ikiwemo                ya kuvisha mataji warembo wasiokidhi vigezo. Chanzo                  cha Habari: Gazeti la Mtanzania,                December 25.