Saturday, December 06, 2014

WATANZANIA WAHOFIA MAISHA KUWA MABAYA IFIKAPO MWAKA 2025



WATANZANIA WAHOFIA MAISHA KUWA MABAYA IFIKAPO MWAKA 2025

Utafiti uliofanywa na   Shirika lisilo la Kiserikali la Twaweza  umebaini kuwa asilimia 46 ya Watanzania wameonyesha wasiwasi  wa mustakabali wa nchi na kuhofia maisha yao kuwa mabaya zaidi ifikapo mwaka 2025.



Aidha,Utafiti huo ulifanyika Agosti, mwaka huu kwa lengo la kupata  takwimu   za sauti ya wananchi kama wana matarajio gani na maisha ya baadaye.

Mtafiti wa Twaweza,Elvis Mushi, akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti kuhusu wananchi wanasemaje kuhusu mustakabali wa nchi yao jijini Dar es Salaam jana, alisema watu 1,408 walihojiwa.

Alisema katika utafiti huo nusu ya wananchi ambao ni asilimia 54 wanafikiria maisha yao kuwa bora ifikapo 2025, mtazamo ambao ulihusisha wakundi yote ya vijana kwa wazee  wa jinsia zote.

Alisema mtazamo huo ni tofauti na mtanzamo wa nchi ya Marekani na Ulaya ambao  wananchi saba kati ya 10 asilimia 65 wanafikiria kuwa watoto wao watakuwa na hali mbaya ya kifedha 2025 kuliko ilivyo sasa.

Mushi alisema wananchi tisa kati 10 wanaamini viongozi wa Tanzania  asilimia 54 au wananchi asilimia 37 watakuwa na uthibiti wa maaamuzi ya nchi yao.

Kwa upande wa utafiti uliofanywa na Shirika la Society for International Development (SID), ilibainisha kuwa uchumi wa Tanzania umepanda lakini umaskini bado unaendelea.

Katika Utafiti huo, mwaka 1990  kiwango  cha umaskini kilikuwa asilimia 39, na mwaka 2007 kilipungua na kufikia asilimia 38 lakini mwaka 2012 kiwango hicho pia kilipungua lakini  bado idadi  ya watu maskini  ni milioni 12.6.

CHANZO: NIPASHE