Saturday, December 06, 2014

NHIF YANYAKUWA TUZO TATU ZA UBUNIFU HIFADHI YA JAMII BARANI AFRIKA



NHIF YANYAKUWA TUZO TATU ZA UBUNIFU HIFADHI YA JAMII BARANI AFRIKA

unnamed1Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee katikati akionyesha tuzo hizo pamoja na washiriki we ngine wa mkutano huo.unnamed3Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee  na washiriki wengine wakiwa katika mkutano huo.unnamed4Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee akiwa na maofisa wengine wa mfuko  huo wakiwa katika picha ya pamoja.unnamed5Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee na washiriki wengine kutoka mataifa mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.unnamed6Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee akielezea jambo katika mkutano huo.unnamed7Mandhari ya jiji la Cassablanca Morocco
……………………………………………………………………………………………….
Mwandishi Maalum Casablanca, Morocco
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF umenyakua tuzo tatu za ubunifu
katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika zinazosimamiwa na
Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani (ISSA).
Halfa ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika Jijini Casablanca nchini
Morocco usiku wa tarehe 3 Desemba, 2014 katika hoteli ya Serana jijini
Casablanca ambapo washiriki zaidi ya 360 kutoka taasisi 75 katika
mataifa 45 ya Afrika zilihudhuria.
Tuzo ambazo NHIF ilikabidhiwa ni katika eneo la utoaji wa huduma za
matibabu za kibingwa maeneo magumu kufika, kazi ambayo mfuko  umefanya
kwa kushirikiana na wataalamu wa hospitali za rufaa nchini. tuzo
nyingine ni katika eneo la TEHAMA katika utayarishaji madai na huduma
za matibabu kwa wanachama wastaafu.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa Kanda ya Afrika ambacho pia
kilijadili mambo muhimu kuhusu sekta ya hifahi ya jamii na kutambua
kazi za ubunifu uliongozwa na Waziri wa kazi Mheshimiwa Gaudensia
Kabaka pamoja na Viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA) na baadhi ya
Watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini.
Tangu kuanza kutolewa kwa ambazo hushindaniwa kila baada ya miaka
mitatu, NHIF imeng'ara mara zote.Mwaka 2008 ilipata tuzo ya cheti cha
heshima cha ubunifu mjini Kigali kwa kuwashirikisha wadau wake katika
utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ngazi ya mkoa. Mwaka 2011
ulikuwa mshindi wa kwanza wa jumla barani Afrika na mwaka huu umeibuka
tena na ushindi huo muhimu unaoitangaza Tanzania kimataifa kupitia
Bima ya Afya.
Mbali ya NHIF, Tanzania pia imengara kwa kuzoa jumla ya tuzo 6 mbapo
Mamlaka ya Udhibiti ya SSRA, Mfuko wa Pensheni wa PPF na Mfuko wa PSPS
pia ilijizolea tuzo moja moja kwa kila mmoja hivyo kufanya Tanzania
kuwa na jumla ya tuzo 6 na kuifanya kuwa kinara katika ukanda wa nchi
za Afrika mashariki na ya Kati.
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika nchi nne ilipata heshima ya pekee
kwa kazi zao za ubunifu. Mifuko hiyo ni kutoka Cameroon yenyewe
iliyonyakua tuzo 8, Gabon, Maurtania, wenyeji Morocco.
Washindi wa jumla wa kwa mwaka 2014 ni wenyeji Morocco na Jirani zao
wa Mauritania ambao kwa pamoja wamepata tuzo ya jumla kwa kutoa huduma
bora, kuongeza uwigo wa wanaonufaika na huduma za mifuko hiyo hasa
wasio na uwezo, matumizi ya TEHAMA na huduma kwa wateja na ufanisi kwa
ujumla