Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi, (NEEC), na TIB Development bank, wametialiana saini makubaliano ambayo yatatoa fursa kwa vijana wahitimu wa vyuo vikuu na vya kati kupata fursa ya mikopo kwa nia ya kujiajiri wenyewe.
Katika makubaliano hayo TIB itatoa mikopo hiyo ambapo kwa kuanzia kiasi cha shilingi bilioni 1 kimetengwa kwa ajili ya mpango huo utakaoratibiwa na NEEC ambayo itakuwa na jukumu la kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana hao ikiwa ni pamoja na kusaidia namna ya kutayarisha andiko, (Proposal), la miradi kwa nia ya kuomba mikopo.
Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya taasisi hizo mbili, mikoipo hiyo itatolewa Tanzania Bara na inalenga kusaidia miradi ya kilimo, uzalishaji, biashara na huduma kwa lengo la kuwawezesha vijana katika harakati za kukuza uchumi wa taifa.
Taarifa hiyo pia ilifafanua kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa vyama vya ushirika (Cooperatives), na mtu mmoja mmoja (Individual), Viwango vya mikopo itakayotolewa kwa mujibu wa taarifa hiyo ni shilingi zisizozidi milioni 200 kwa SMEs na washirika au ushirika, wakati shilingi zisizozidi milioni 50 kwa kijana mhitimu wa chuo kikuu mjasiriamali ambaye awe amefaulu mafunzo hayo ya kuwaandaa wajasiriamali yatakayokuwa yakitolewa na NEEC.
Picha ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEEC), Dkt. Anacleti Kashuliza, (Kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Peter Noni, wakionyesha waandishi wa habari mikataba hiyo baada ya kuisaini.
Noni wa TIB, (Kulia) na Dkt. Kashuliza wa NEEC, wakibadilishana hati hizo baada ya kusaini
Katibu mtendaji wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi, NEEC, Dkt. Anacleti Kashuliza, (waliokaa kushoto) na mkurugenzi mtedaji wa benki ya maendeleo TIB, Peter Noni, wakisaini makubaliamo hayo. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni afisa wa sheria wa NEEC, Esther Barikie Mbaga, Mwenyekiti wa bodi ya NEEC, Omar Issa, mkurugenzi wa mfuko wa uwezeshaji wa TIB, Prisca V. Chang'a, na mwanasheria na katibu wa bodi ya TIB, Martha J.J.Maeda
"Vijana wasajili kampuni zao kwwnye mamlaka zinazohusika ili iwe rahisi kuaminiwa na benki" Peter Noni
"Kuwawezesha wananchi kiuchumi ndio njukumu letu kuu" Dkt. Anacleti Kashuliza
Shahidi upande wa TIB, ambaye ndiye mwanasheria wa benki hiyo, Martha J.J.Maeda, "akimwaga wino"
Afisa wa sheria wa NEEC, Esther Barikiel Mbaga, akithibitisha kwa kuweka saini yake kuwa makubaliano hayo ni ya kisheria na halali
Baadhi ya viongozi wa TIB, wakifurahia jambo
Picha ya pamoja ya waliohudhuria hafla hiyo