Monday, December 22, 2014

MIHIMILI MITATU ISIPOELEWANA NCHI HAIWEZI KUTAWALIKA - UTOUH


MIHIMILI MITATU ISIPOELEWANA NCHI HAIWEZI KUTAWALIKA - UTOUH
Na Bakari Issa,Dar es Salaam

ALIYEKUWA Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG),Ludovick Utouh amesema mihimili mitatu iwekewe mipaka na kuangalia isiingiliane katika utendaji wake wa kazi kuruhusu kwake kuingiliana ni kufanya serikali isitawalike.

Hayo amesema leo jijini Dar es Salaam katika kupokea tuzo ya uadilifu kutoka kwa Kampuni ya Dream  Success Enterprises kutokana na kutambua umuhimu wa utendaji wake wa kazi.

Alisema kuwa mihimili mitatu isipojua mipaka yake itawaweka wananchi washindwe kujua uwepo wa mihimili hiyo na kufanya nchi ishindwe kutawalika kutokaka na mihimili hiyo kuwa na mianya ya kutoafikiana katika utendaji..

Utouh alisema kuna vitu hataweza kusahau katika ofisi ya CAG moja ni fedha zilizochotwa katika akaunti za nje (EPA) pamoja na ripoti ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, David Jairo ambapo wabunge walishindwa kujua uhalali wa fedha zilizochangishwa  na Jairo na hakuna sheria yeyote iliyovunjwa.

"Tuzo hii nimepata lakini nimepita  katika kipindi ambacho jina la ufasadi limeweza kuzaliwa kutokana  na uchotaji wa fedha za EPA na kufanikisha zingine kuweza kurudi, nchi zingine huwa zinashindwa kabisa kurudisha fedha za namna hiyo"alisema Utouh.