Friday, December 05, 2014

Membe mgeni rasmi mahafali UB, kufanyika kesho Bagamoyo



Membe mgeni rasmi mahafali UB, kufanyika kesho Bagamoyo
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, kesho Jumamosi Desemba 6 anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi Katika Mahafali ya Pili ya  Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo kwa vyombo vya Habari Dar Es Salaam,  na Ofisa Habari wa  ( UB), Happiness Katabazi, inasema Kuwa Membe ndiye Atakuwa mgeni rasmi Katika mahafali hayo ambayo yatafanyika Katika Hoteli ya Kiromo  View Resort  kijijini Kiromo Wilayani Bagamoyo,Mkoani Pwani.


Katabazi alisema jumla ya wahitimu 99 wanatarajiwa kutunukiwa Vyeti Katika ngazi ya Shahada ya Uzamili, Shahada ya Kwanza, Diploma,  na cheti.


Wakati huo huo , Juzi Makamu wa Rais  Dk.Mohammed Gharib Bilal alishindwa kuhudhuria sherehe za uwekwaji  wa jiwe la Msingi wa makazi ya kudumu ya UB ikiwa ni ishara ya kuanza kwa ujenzi wa makao makuu ya UB kijijini hapo ambapo ujenzi ukikamilia majengo hayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 5000, yaliyopaswa yafanyike Katika kijijini Cha Kiromo ,Bagamoyo Mkoani Pwani kwasababu alikuwa amebanwa na majukumu mengine ya Kitaifa na akaomba apangiwe tarehe nyingine ya kuja kuweka jiwe Hilo la Msingi.


Akizungumza na waandishi wa Habari Katika kijijini Kiromo Juzi wakati akiiarisha sherehe za Utiaji wa jiwe la Msingi , Makamu Mkuu wa UB, Profesa Costa Ricky Mahalu alitoa historia fupi la shamba Hilo lililopo Kijijini Kiromo Alisema  familia yake ililinunua rasmi Agosti 26 Mwaka 2003.

 
Profesa Mahalu alisema Katika shamba Hilo familia yake imeamua kukata heka 100 na kuzitoa kwa UB ili UB iweze kujenga makazi yake ya kufumu katika Kijiji cha Kiromo na kwamba heka nyingine zilizosalia familia yake itazitoa  kwa Taasisi nyingine za elimu ya juu  na kwamba Tayari Taasisi nne za elimu ya juu ikiwemo Chuo Kikuu Kimoja Cha kigeni kimeishaonyesha nia ya kutaka Kuja Kujenga Taasisi yake ya elimu Katika shamba Hilo.


Profesa Mahalu Alisema shamba hilo kabla familia yake haijalinunua lilikuwa likimilikiwa na lililokuwa shirika la Serikali la NAFCO na baada ya kufirisika mwaka 1990  lilichukuliwa na LART  ambaye alikuwa na jukumu la kuchukua  kuuza Mashitaka ya serikali yalikuwa na matatizo ya kifedha.


' LART ikamkabidhi  kampuni ya PHLLIP&Ltd  iliyauza mashamba matatu  ya NAFCO  yaliyopo Kiromo. Hayo mashamba matatu ,Moja iliuziwa familia ya Mahalu na mkataba wa mauzo wa shamba Hilo la Mahalu na LART ulisainiwa Agosti 26 Mwaka 2903  na baada ya hapo  umiliki wa shamba  unachukuliwa  na familia ya Mahalu kwa mujibu wa Sheria.' Alisema Balozi Mahalu.