Friday, December 19, 2014

Kampuni ya Simu Tanzania TTCL Yazinduwa Dili la Ukweli



Kampuni ya Simu Tanzania TTCL Yazinduwa Dili la Ukweli
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imezinduwa huduma mpya kabambe ambayo inampa mteja wa kapuni hiyo fursa ya kufurahia modem ya bure na vifurushi vya intaneti kwa bei nafuu, huduma ambayo imetolewa kama ofa kwa wateja hasa katika kuelekea siku kuu za Chrismas na Mwaka mpya.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam juu ya huduma hiyo, Meneja Huduma za Intaneti wa TTCL, Abdul Mombokaleo amesema kampuni ya Simu Tanzania imeamua kuzindua promosheni mpya ya "DILI LA UKWELI" inayotoa fursa ya mteja wa TTCL kufurahia huduma ya intaneti kwa bei nafuu zaidi na kujipatia modem.

"...TTCL siku ya leo imezindua promosheni mpya ya "DILI LA UKWELI" inayotoa fursa ya mteja wa TTCL kufurahia huduma ya intaneti kwa bei nafuu zaidi na kujipatia modem ya bure.

Akifafanua zaidi Mambokaleo alisema promosheni hiyo mpya ya "Dili la Ukweli" inatoa fursa kwa wateja kufurahi modem ya bure pamoja na vifurushi ambavyo vimepunguzwa bei kwa kiwango ambacho Mtanzania wa kawaida anaweza kuimudu.

Aidha akifafanua juu ya utaratibu wa promosheni alisema ili mteja apate modem ya bure Mteja atapaswa kununua intaneti bila kikomo kwa shilingi 20,000/- tu ambayo itatumika ndani ya mwezi mzima na huduma hiyo ni kwa wateja wapya tu. 

"...Kwa mteja wenye modem tumewapa fursa ya kuchagua vifurushi ambavyo vimepunguzwa bei. DILI LA UKWELI inatoa fursa kwa wateja kufurahia punguzo la bei ya vifurushi vya intaneti vya siku, wiki na mwezi kwa bei nafuu sana. Intaneti ya TTCL inaubora, ina kasi na uwakika, kwani teknolojia inayotumika ni ya kuaminika zaidi. Katika kuhakikisha wateja wa huduma ya intaneti wanafurahia zaidi, TTCL imeshusha bei ya intaneti ili kuendelea kukidhi mahitaji ya wateja wake.
Meneja wa Bidhaa za Intaneti wa TTCL, Abdul Mombokaleo (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani), kulia ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa TTCL, Laibu Leonard na Kushoto ni Ofisa habari wa TTCL.
Meneja wa Bidhaa za Intaneti wa TTCL, Abdul Mombokaleo (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) , anayefuata ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa TTCL, Laibu Leonard.