Mwalimu wa shule ya sekondari ya mazungwe Revania Ndebigeze(39)Wilaya ya Uvinza Mkoani hapa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Kigoma(Maweni)baada ya kuungua vibaya na moto wa gesi.
Akiongea na mwandishi wa habari hii kwa taabu katika chumba cha upasuaji mwalimu huyo alisema kuwa tukio hilo lilimkuta jumatatu majira ya saa tano asubuhi wakati akijiandaa na mapishi nyumbani kwake.Alisema kuwa alikuwa ametoka kazini na kupita kwenye maduka ya gesi kigoma mjini na kununua gesi na kupewa maelekezo yote na wataalum ya jinsi ya kuitumia gesi hiyo.
Alipofika nyumbani aliungaunisha gesi hiyo na jiko ili aweze kutumia lakini alishindwa na kumuita mwalimu mwenake amsadie lakini naye alishindwa kufanikiwa kuliwasha jiko hilo.
''Niliamua kujaribu tena kuliwasha mwenyewe kulinga na maelezo niliyopewa na taalamu wakati na nunua nikafanikiwa kuliwasha lakini haikupita dakika tano nikasikia harufu ya tofauti nikaamua kwenda kulizima ndo likalipuka na kuniunguza ''alisema mwalimu huyo kwa masikitiko.
Alisema baada ya gesi kulipuuka na kumuunguza majirani walimpeleka katika zahanati ya jirani ya mazungwe ambapo alipatiwa rufaa ya kwenda hospita ya rufaa ya maweni anapopatiwa matibabu mpaka sasa.Mwalimu huyo ameungua vibaya sehemu za usoni, miguu yote na mikono yote,mabega,mikono,
Daktari wa zamu Dkt Fadhili Kabaya alisema hali ya mgonjwa inaendelea vizuri.