Sunday, December 07, 2014

JESHI LA POLISI-KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI NA VODACOM WAENDESHA ZOEZI LA UTOAJI ELIMU NA UPIMAJI WA VILEVI MWILINI KWA MADEREVA



JESHI LA POLISI-KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI NA VODACOM WAENDESHA ZOEZI LA UTOAJI ELIMU NA UPIMAJI WA VILEVI MWILINI KWA MADEREVA
 Afisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Steven Mwakibolo kwa kutumia kifaa maalum wakati wa upimaji madereva ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani  inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia, akifuatilia kwa karibu zoezi hilo lililofanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, akimuelimisha dereva wa basi liendalo mkoani Elias Samu kuhusiana na pete ya kidoleni inayotolewa na Vodacom Tanzania kwa ushirikiano na jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani yenye ujumbe "Wait To Send" unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam katika mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani inayodhaminiwa na kampuni hiyo.
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed Mpinga akiwafafanulia jambo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kushoto) wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Hamza Kassongo na  Henry M. Bantu wakati wa zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani lililofanyika leo katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam. Zeozi hilo ni mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani  inayodhaminiwa Vodacom Tanzania.
 Maafisa wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakimsomea dereva wa basi la kwenda mikoani matokeo yake ya vipimo vya kilevi mwilini wakati wa zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi lililofanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam,anaeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia ambapo kampuni yake ni wadhamini wa kampeni ya Usalama Barabarani.
 Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Mzee Hamza Kassongo pamoja na maafisa wa Vodacom Tanzania wakionyesha pete zenye ujumbe wa "Wait to Send" wakati wa zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani lililofanyika leo katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani  inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania. Pete hizo ziligawiwa kwa madereva wa mabasi yaendayo mkoani zikiwa na ujumbe huo unaowakumbusha kusubiri hadi wakiwa wamesimamisha vyombo hivyo ndipo watumie simu zao za mkononi.
Afisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la mkoani, Elias Samu kwa kutumia kifaa maalum wakati wa zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani katika mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani  inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, akifuatilia kwa karibu zoezi hilo liliofanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.