Monday, December 22, 2014

ADHA YA USAFIRI JIJINI DAR


ADHA YA USAFIRI JIJINI DAR
 Abiria katika moja ya Daladala linalofanya safari zake kati ya Mbezi - Posta wakigombea kuingia kwenye gari hilo kupitia mlango wa Dereva,baada ya Kondakta wa Basi hilo kutofungua mlango kutokana na uwingi wa abiria hao.tukio hili limetokea jioni hii katika kituo cha Daladala cha Posta Mpya,jijini Dar es Salaam.
 Mara Dereva akashukia mlango wa abiria na kuja kuwazuia abiria kupanda basi hilo kupitia mlango wake,hapo napo ilikuwa mbinde ile mbaya.
 Mara akafanikiwa kuwadhibiti na kuwataka abiria wote kwenda kwenye mlango husika.