Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akikata utepe kama ishara ya kukabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu wenye ulemavu, wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), kwa ajili kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamari, katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Buguruni Viziwi jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya na (kulia) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Abubakar Rakesh na mnufaika wa kibanda hicho, Hebron Mwansele (kwenye baiskeli).
Sehemu wa wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akihutubia wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa HREDP, Abubakar Rakesh akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (kushoto), akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Naibu Waziri Makamba.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akikagua kioski baada ya kukabidhi.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akiwatunza pesa wanamuziki ya walemavu ya Bendi ya Tunawajali, iliyokuwa ikitumbuiza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akijadiliana jambo na baadhi ya wanachama wa HREDP.
Katika kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imekabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu wenye ulemavu yenye lengo la kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamali
Sambambal na hilo Airtel pia imewapatia mtaji wa kuanzisha biashara ili kuwawezesha watakao nufaika na vibanda hivyo kuwa mawakala wa huduma ya Airtel money na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel kupitia vibanda hivyo vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Saalam.
Akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano , Naibu Waziri wa mawasiliano Mh. Januari Makamba alisemaâ tunapenda kuwashukuru Airtel kwa kutanua wigo na kutoa msaada kwa watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi. Serikali yetu iko makini katika kuhakikisha kila mtanzania anapata haki sawa bila kubagua makundi natoa fulsa sawa katika maeneo mbalimbali.
Sisi kama Serikali tunaamini msaada mliopokea leo utakuwa chachu ya kuleta maendeleo ya kiuchumi na nyenzo kwa wanachama wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu kujikwamu na tatizo la kiuchumi unaowakumba makundi mengi kama haya katika jamiiâ.
Sera ya serikali kwa walemavu inalenga kuboreshea mazingira watu wenye ulemavu na kuwahusisha katika shughuli za uzalishaji ili kuinua uchumi na kutumia kwa ufanisi rasilimali zilizopo katika kuboresha huduma. Naaamini kwa Airtel kuwekeza kwenye jamii leo hakutachangia kuboresha maisha ya wengi tu bali kutachangia kutekeleza na kutilia mkazo agenda za Serikali.
Nachukua fulsa hii kuwaomba makampuni mengine na wadau mbalimbali kushirikiana na serikali katika kutoa misaada ya muda mrefu na endelevu katika makundi mengine kama haya nchini kama ilivyofanywa na Airtel leoâ. Aliongeza Makamba
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bibi Beatrice Singano alisema â kwa mara nyingine tena tumefikia jamii kupitia mpango wetu wa huduma kwa jamii tukiamini kwa kufanya hivi tunachangia na kusaidi familia za wanachama wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu , pamoja na kuinua uchumi kwa watu wenye ulemavu kwa ujumla. Airtel tunatoa fulsa na kuwawezesha wale waliokuwa na ndoto za kumiliki biashara zao kuweza kuzifikia ndoto hizo na kujikita kwenye ujasiriamali na biashara.
Tunaamini Msaada huu haujalenga kuwapatia mtaji tu bali vifaa vya kuendesha biashara pamoja na mafunzo ya jinsi ya kuendesha biashara endelevu. Tunauhakika ushirikiano tulioanzisha leo utawaweza wanachama wa kikundi hiki kuwa sehemu ya kutoa huduma zetu na hivyo kupata faida itakayowawezesha kuwa wajasiriamali bora nchiniâ.
Tunawaasa wale wote watakaofaidika na msaada huu leo kutumia vibanda hivi kwa ubunifu na kuhakikisha vinawanufaisha kufikia malengo yao ,bado tutaendelea kushirikiana pamoja nanyi na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha tunatimiza lengo letu la kuboresha maisha ya watanzania kupitia huduma na bidhaa zetu za kibunifu na fursa za kibiasharaâ aliongeza Singano.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu Bw. Abubakar Rakesh alisemaâ tunayofuraha kuona baadhi ya wenzetu wakiwezeshwa kupata rasilimali muhimu za kuanzisha biashara.
Tunawashukuru Airtel kwa msaada huo na kwa kukiwezesha kikundi hiki kuwa cha kwanza kupata msaada kama huu . Wito wangu kwa wanachama wenzangu ni kutumia nafasi hii vizuri, kuweka jitihada katika kazi zao ili kufanya vyema na kufanikiwa katika biashara zaoâ.
âNapenda kutoa shukrani zangu za pekee kwa serikali na kwa Mh Makamba,kwa mchango wake na kujitolewa kwake kuwasaidia watu wenye ulemavuâ aliongeza Rakesh