Tuesday, November 18, 2014

TRA yaendelea na Maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi Tanzania,Yatoa Msaada Hospitali ya Temeke na Kukabidhi Madawati 100 Shule ya Msingi Misitu,Kivule



TRA yaendelea na Maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi Tanzania,Yatoa Msaada Hospitali ya Temeke na Kukabidhi Madawati 100 Shule ya Msingi Misitu,Kivule
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),leo Novemba 18,2014 walitembelea Hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam,ambapo waliweza kutoa msaada wa vitu mbali mbali kwa watoto waliolazwa Hospitalini hapo pamoja na kukabidhi baadhi ya vifaa vya Usafi kwa Uongozi wa hospitali hiyo Mbali na kukabidhi vifaa hivyo,pia walijumuika pamoja na kujitolea kufanya usafi wa Mazingira ya Hospitali hiyo.

Mara baada ya kukamilisha shughuli zote za hospitalini hapo,Wafanyakazi hao walielekea moja kwa moja katika Shule ya Msingi Misitu,ilipo katika Kata ya Kivule,Kitunda na kuweza kukabidhi msaada wa Madawati 100 ambayo yatapunguza adha ya kukaa chini kwa asilimia 74 ya wanafunzi wote wa shule hiyo ambao idadi yake imefikia 590.

Hapo awali wanafunzi hao wote walikuwa wakikaa chini na kuendelea na masomo yao.

TRA imefikia kufanya hivyo,ikiwa katika muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi chenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti" ambayo kilele chake ni Novemba 21,2014 huku Mgeni Rasmi akitazamiwa kuwa Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kanda ya Temeke,Victor Msuya (kulia) akizungumza na mmoja wa wauguzi wa zamu katika Wadi ya Watoto ya Hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Novemba 18,2014,wati Timu TRA ilipotembelea Wadi hiyo.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kanda ya Temeke,Victor Msuya (kulia) akiwaongoza maafisa wengine wa TRA kutoa bidhaa mbali mbali walizokwenda kuwagawia watoto wanaopatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Temeke,Jijini Dar es Salaam leo Novemba 18,2014.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakijadiliana jambo wakati wakijiandaa kwenda kufanya usafi wa Mazingira wa Hospitali ya Temeke,Jijini Dar es Salaam leo Novemba 18,2014.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Misitu,Ilipo katika kata ya Kivule,Kitunda jijini Dar es Salaam wakiwa wameketi kwenye madawati mapya yaliyokabidhiwa leo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Nyuma yao ni Baadhi ya Maofisa wa TRA waliofika shuleni hapo. 
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Misitu,Hyasinta Hugo akizungumza wakati akiukaribisha Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Shuleni hapo. 
 Mkurugenzi wa Walipakodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard Kayombo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki kuzungumza na uongozi wa Shule hiyo na kukabidhi madawati.
 Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akizungumza na uongozi wa Shule hiyo pamoja na wanafunzi kabla ya kukabidhi madawati,yaliyotolewa na TRA kwa shule hiyo.
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akipena mkoni na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Misitu,Hyasinta Hugo wakati akimkabidhi madawati 100 yaliyotolewa na TRA kwa shule hiyo.