Tanzania leo                imekabidhiwa rasmi Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la                Afrika Mashariki baada ya Kenya kumaliza muda wake wa                kipindi cha mwaka mmoja. 
        Waziri wa Wizara ya                Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta na Katibu                Mkuu Bi. Joyce Mapunjo walipokea Uenyekiti huo katika                Mkutano wa Baraza wa Mawaziri uliofanyika leo katika                Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC), Jijini                Nairobi, Kenya. 
         Rais wa Tanzania                anatarajiwa kupokea Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika                Mashariki siku ya Jumapili katika Mkutano wa 16 wa Wakuu                wa Nchi za Jumuiya utakaofanyika pia hapa KICC. 
                Waziri Samuel Sitta                  akizungumza baada ya kupokea Uenyekiti wa Baraza la                  Mawaziri la Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki leo 
                Katibu Mkuu wa Wizara                  ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo                  akisoma taarifa ya Kamati ya Makatibu Wakuu wa Nchi za                  Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Baraza la Mawaziri.                  Wengine kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika                  Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera, Waziri Mh.                  Samuel Sitta na Mwandishi wa Taarifa za Mikutano Mpya                  kutoka Uganda Bi. Mary Nankabirwa.
                Mwenyekiti anayemaliza                  muda wake Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Kenya                  Bi. Phyllis Kandie (katikati) kabla ya kukabidhi                  uenyekiti kwa Waziri Samuel Sitta wa Tanzania. Kushoto                  ni Bw. Mugisha Kyamani kutoka Tanzania ambaye alikua ni                  Mwandishi wa Taarifa za Mikutano kwa kipindi cha mwaka                  mmoja uliopita
        Waziri                  wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel                  Sitta akliwa na  Waziri wa Biashara na Viwanda wa                  Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), Waziri Ofisi                  ya Rais Utawala Bora Mh. George Mkuchika (wa pili kulia)                  na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh.                  Dkt. Abdullah Juma Saadalla (kulia).
                Waziri                  wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel                  Sitta (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na Naibu                  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki                  anayeshughilikia Miundombinu Dkt. Enos Bukuku                  walipokutana Jijini Nairobi kabla ya kuanza kwa Mkutano                  wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki leo. Wengine                  ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Mh. Nassor                  Ahmed Mazrui (kushoto), Waziri Ofisi ya Rais Utawala                  Bora Mh. George Mkuchika (wa pili kulia) na Naibu Waziri                  wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt. Abdullah                  Juma Saadalla (kulia).
        .jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)