Thursday, November 20, 2014

MKUU WA WILAYA TEMEKE ASHAURI VODACOM KUSAMBAZA ZAIDI HUDUMA KWA WATEJA WAKE.



MKUU WA WILAYA TEMEKE ASHAURI VODACOM KUSAMBAZA ZAIDI HUDUMA KWA WATEJA WAKE.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke Shophia Mjema wa kwanza (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.Hafla hiyo imefanyika leo.
 Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(katika)akimfafanulia jambo kuhusiana na simu aina ya Vodafone smart kicka Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema(kulia) alipofika  kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
 Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kushoto)na Matina Nkurlu Meneja uhusiano wa kampuni hiyo(katikati)wakimsikiliza jambo kwa umakini Mkuu wa Wilaya ya Temeke Shophia Mjema(kulia)mara baada ya kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke Shophia Mjema wane toka kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania mara baada ya kuzindua duka jipya la kampuni hiyo lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam leo.

=========  =======  ========
Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema ametoa ushauri kwa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kufungua zaidi  vituo vya kutoa huduma kwa wateja wilayani humo ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.Alitoa ushauri huo wakati akifungua duka la Vodacom la Mbagala ambapo pia alitoa pongezi kwa hatua hiyo.
 
Katika kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Mbagala na maeneo jirani ya Mtoni,Temeke na Tandika  wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imefungua duka jipya  katika  eneo la Mbagala Zakiemu.

Mbagala ni moja ya kitongoji maarufu katika cha jiji la Dar es Salaam ambacho kinakuwa kwa kasi kwa maendeleo na kuwa kivutio cha wawekezaji wengi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu na shughuli mbalimbali za kibiashara ikiwemo kituo kikubwa cha mabasi yanayoelekea mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara.

Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma  kwa mawakala wa Mpesa na uuzaji wa bidhaa  za Vodacom na litawawezesha wateja wa  Mbagala na vitongoji vyake   wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa ya Kusini  na wateja kutoka maeneo ya Temeke,Kurasini,Mtoni  na Tandika.Mtandao wa Vodacom unaongoza  kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika wilaya ya Temeke.

Hassan Saleh Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Vodacom Tanzania,alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa  ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza  kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya  ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.

"Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu."Anasema Saleh.


Vodacom ina mtandao wa maduka  84 nchi nzima na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake nchini na  duka lililofunguliwa leo ni la 5 kufunguliwa katika wilaya ya Temeke.