Wednesday, November 05, 2014

MH. MAKINDA AWASILI NA KUPOKELEWA KWA SHANGWE NA VIONGOZI WA UWT KWA KUCHAGULIWA KUWA RAIS WA BUNGE LA SADC


MH. MAKINDA AWASILI NA KUPOKELEWA KWA SHANGWE NA VIONGOZI WA UWT KWA KUCHAGULIWA KUWA RAIS WA BUNGE LA SADC
Rais wa Jukwaa la Wabunge wa SADC (SADC PF) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Anne Makinda akilakiwa kwa shangwe na Viongozi wa UWT mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jana Usiku ikiwa ni furaha za kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jukwaa la Bunge la SADC mjini Victoria Falls, Zimabwbe.
Rais wa Jukwaa la Wabunge wa SADC (SADC PF) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Anne Makinda akipokea shada la Maua kutoka kwa Bi. Riziki Kingwande, Mkuu wa Idara ya Organisaztion ya UWT.
Katibu wa UWT Mhe. Amina Makilagi akisoma salam za Pongezi kwa niaba ya UWT.
Rais wa Jukwaa la Wabunge wa SADC (SADC PF) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Anne Makinda akiwapongeza viongozi wa UWT kwa mapokezi Makubwa waliyomfanyia.Picha na Owen Mwandumbya