Tuesday, November 11, 2014

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA



MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA
Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Moshi vijijini  ,Hussein Jamal akizungumza wakati wa kikao cha makatibu kata na makatibu wa matawi kilichofanyika katika hotel ya King Size Himo.
Mwenyekiti wa Makatibu katika jimbo la Vunjo ,Shaban Mwangi akisoma taarifa ambayo inadaiwa kupikwa kwa lengo la kukivuruga chama hicho katika jimbo la Vunjo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini Miriam Kaaya akizungumza wakati wa kikao hicho ambacho kilijadili pia tuhuma zilizotolewa dhidi yake.
Naibu kamanda wa vijana wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Shirima akizungumza wakati wa kikao hicho kilichokuwa na lengo la kurudisha hali ya amani na umoja ndani ya chama cha mapinduzi jimbo la Vunjo.