Monday, November 10, 2014

BALOZI MDOGO WA TANZANIA DUBAI MHE. OMAR MJENGA, AKUTANA MTENDAJI MKUU NA RAIS WA FLYDUBAI



BALOZI MDOGO WA TANZANIA DUBAI MHE. OMAR MJENGA, AKUTANA MTENDAJI MKUU NA RAIS WA FLYDUBAI
Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Ghaith Alghaith, Mtendaji Mkuu na Rais wa Shirika la Ndege la Flydubai katika ofisi za shirika hilo. Katika mazungumzo, Mhe. Omar Mjenga, amemueleza kuhusu maombi ya Serikali ya Tanzania kwa shirika hili ya kuingia ubia na Air Tanzania kwa ajili ya safari za ndani (domestic flights) na zile za kikanda (regional fligjts). Nia ya mpango huu ni kuiwezesha Air Tanzania kuanza safari zake zote za ndani na kikanda zilizosimama kwa kukosa ndege za kufanya safari hizo. Hivyo basi ushirikiano utakuwa ukiutwa: Air Tanzania Operated by Flydubai. Kwa mpango mashirika yote yataingia mkataba wa kugawanya mapato kwa asilimia watayokubaliana.
Balozi Mdogo wa Tanzania -Dubai,Mhe. Omar Mjenga akiwa katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Flydubai Mhe. Ghaith Alghaith katika ofisi za flydubai.
Balozi Mdogo wa Tanzania -Dubai,Mhe. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Ghaith Alghaith, Mtendaji Mkuu wa shirika la ndege la Flydubai ambalo limezindua safari zake kati ya Dubai na Far es salaam kuanzia tarhe 16 Oktoba 2014 kwa nauli ya dola 399 Dubai-Dar-Dubai.