Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro akiongoza gari ya Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye kijiji cha Elang'atadapash wilayani Longido kuzindua mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na UNDP.
Na mwandishi wetu
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amewataka wananchi wa Longido kwa kushirikiana na viongozi wao kutunza vyanzo vya maji katika wakati huu ambapo mabadiliko ya tabia nchi yanafanya maeneo mengi kuwa makame.
Alvaro alisema hayo wakati akizindua mradi mkubwa wa maji wa kwa vijiji vya Noondoto na Elang'atadapash uliosaidiwa na UNDP ambao unahudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.
Mratibu huyo alisema kwamba utunzaji wa vyanzo vya maji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 92 utawezesha wanawake kuendelea kushiriki katika kazi nyingine za jamii badala ya kuhangaika kutwa kusaka maji.
Aidha alisema viongozi wanatakiwa kuendelea kutoa elimu wa kutunza vyanzo vya maji na mradi huo ili uwe endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akiongozana na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro (kulia) mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Elang'atadapash tarafa Kitumbeine wilaya ya Longido mkoani Arusha kuzindua mradi mkubwa wa maji uliosaidiwa na UNDP ambao utahudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.
Aliwashukuru wakazi wa eneo hilo kwa kuthamini na kutambua kwamba mradi huo ni wao na hivyo kuamini kwamba watafanya kila waliwezalo kuutunza hasa kwa kuzingatia matatizo yaliyopo sasa ya ukame na mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi huo ambao ulifanyiwa kazi na shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists initiative,baada ya kupata ruzuku ya UNDP umelenga kuboresha maisha ya watu, afya ya mifugo na wanyamapori kwa kuwapatia maji safi na salama.
Aidha fedha zilizotolewa na UNDP zimefanyakazi ya kujenga tangi la mita za mraba 45 katika kijiji cha Elang'atadapash,matangi ya kuvuna maji ya mvua matano na kila moja likiwa na mita za mraba tatu, ukarabati wa matangi matatu ya kuwezesha msukumo wa maji,kukabarati vituo vya kuchotea maji vinne na kufundisha vyama vya ushirika vya watumia maji 10 katika kata za Ketumbeine, Elang'atadapash na Iloirienito zilizopo wilayani Longido.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisalimiana na wanawake wa Kimasai wa kijiji cha Elang'atadapash alipowasili kijijini hapo kuzindua mradi wa maji unaofadhiliwa na UNDP.
Aidha wananchi wamefunzwa namna ya kufanya menejimenti ya maji.
Katika risala yao iliyosomwa na Mike Olemokoro wa Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists initiative IPI Tanzania, wananchi hao pia wamesema mchango wao wa kazi na pia wa halmashauri katika masuala ya kiufundi yamechukua asilimia 40.
Maji hayo yanatarajiwa kuwasaidia wananchi wa kata za Ketumbeine, Elang'atadapash na Iloirienito.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na mmoja wakazi wa kijiji hicho aliyefika kumlaki. Kulia ni Diwani wa viti maalum kata ya Elang'atadapash wilayani Longido Naini Mokoro.
Na hili ndio tangi la mita za mraba 46 katika kijiji cha Elang'atadapash lililojengwa na UNDP kwa ajili ya kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji hicho ambalo litahudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.
Mratibu Kitaifa kutoka UNDP, Bw. Nehemia Mususuri akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Katikati ni Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro.
Kikundi cha wakinamama wa Kimasai wakitoa burudani kwa mgeni rasmi kabla ya kuzindua mradi huo wa maji.
Meza kuu.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro (mwenye shati jekundi) wakisoma risala pamoja na mkalimani wa lugha ya Kimasai kwa mgeni rasmi Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Diwani wa viti maalum kata ya Elang'atadapash wilayani Longido Naini Mokoro, akimvisha kikoi Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kama shukrani ya jamii ya wafugaji na wakazi wa kata hiyo.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akipokea fimbo yenye heshima ya uchifu wa kimasai kutoka kwa Diwani wa viti maalum kata ya Elang'atadapash wilayani Longido Naini Mokoro.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipozi na baadhi ya wakina mama wa Kimasai wa kijiji cha Elang'atadapash.
Pichani juu na chini ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikata utepe kuzindua rasmi mradi mkubwa wa maji wa kwa vijiji vya Noondoto na Elang'atadapash uliosaidiwa na UNDP. Kushoto ni Mratibu Kitaifa kutoka UNDP, Bw. Nehemia Mususuri akishuhudia tukio hilo.
Jiwe la msingi kama linavyosemeka pichani.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wakazi wa vijiji vya Noondoto na Elang'atadapash mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akinawa mikono na maji hayo mara baada ya kuzindua rasmi tangi kubwa la maji kijijini hapo.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa jiji cha Elang'atadapash, Bi. Nabulu Kumokndare kama ishara ya kuzindua rasmi mradi huo.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akikagua kisima cha maji cha kijiji hicho.
Wanyama wakinywa maji safi na salama wakati wa sherehe za kuzinduliwa rasmi kwa mradi mkubwa wa maji utakaohudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.
Mbuzi wakinywa maji kwenye josho maalum litakalotumika kuhudumia mifugo ya vijiji hivyo.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akizungumza na wakazi vijiji vya Noondoto na Elang'atadapash ambapo aliwaasa kutunza mradi huo kwani maji ni uhai.
Mzee wa kijiji cha Elang'atadapas, Miaroni Lailuda akimwombea dua na baraka Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez pamoja na shirika lake kwa msaada huo.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua mradi huo.