Monday, November 10, 2014

TANZANIA TAYARI KUHIFADHI WALIOACHILIWA ICTR


TANZANIA TAYARI KUHIFADHI WALIOACHILIWA ICTR
Serikali ya Tanzania imeeleza kuwa inao uwezo wa kuwapa hifadhi ya kudumu Raia wa Rwanda waliochiwa huru na mahakama ya kimataifa ya mauaji ya ya Rwanda ICTR iliyoko mjini Arusha iwapo itaombwa kufanya hivyo.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Makamu wa Rais wa Tanzania Dr Mohamed Gharib Bilal katika kilele cha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa mahakama hiyo mnamo mwaka 1994.
Taarifa hii ni ya mwandishi wa BBC Erick David Nampesya kutoka Arusha.
Chanzo: BBC