Saturday, October 04, 2014

Kumbukumbu



Kumbukumbu
Mama Katherine Saguti Lawrence 
 Septemba 22, 1936 - 4 Oktoba 2009

Kete, Mama na Bibi, hujaondoka kamwe miyoyoni mwetu. Upendo wako uliotuachia umekuwa alama isiyofutika miyoyoni mwetu na sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Tunajisikia upo nasi kiroho hususani kupitia upendo huo, kupitia jamii uliyoijali siku zote na kwa maisha yako hapa duniani.

Kete, Mama na Bibi, tunajua tutakuwa na wewe siku moja ambapo sisi wote "tutafurahi na kucheka" pamoja. Ingekuwa heri kama ungekuwa hapa na sisi, lakini ni jinsi Baba Mungu amlivyo panga na tunaendelea kumshukuru na kumtukuza kwa maisha yako nasi. 

Miaka mitano imepita na bado tunajifunza kutokuwa na wewe kimwili, ingawa tunajua kwamba una furaha nyumbani kwa Baba  na unashangilia pamoja na watakatifu na malaika. 

Tunamuomba Mungu atuwezeshe tuweze kuamini na kujitoa kama wewe ulivyoilinda imani na  kujitoa na tuendelee kuwa imara katika imani na "upendo 

Tunakukosa sana, lakini tuna imani miyoyoni mwetu  kwamba siku moja sisi wote tutakuwa pamoja, na huzuni yoyote itabadilika na kuwa furaha na shangwe tukifurahi pamoja na Baba yetu wa mbinguni! 

Unakumbukwa daima na mpenzi  Mume wako, Lawrence Saguti Shelukindo, Watoto na wenzi wao, wajukuu na vilembwe, familia nzima, majirani na marafiki. 

Mungu aendelee kuilaza Roho yako Mahali Pema Peponi, Amina 

Yohana 11: 25 Yesu akamwambia, "Mimi ndiye ufufuo na uzima; mtu akiniamini mimi, hata akifa ataishi;