Friday, October 03, 2014

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI TANZANIA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA ULINZI WA AMANI KWA MAAFISA MAGEREZA TOKA NCHI ZA SADC, MKOANI KILIMANJARO


KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI TANZANIA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA ULINZI WA AMANI KWA MAAFISA MAGEREZA TOKA NCHI ZA SADC, MKOANI KILIMANJARO

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati meza Kuu) akisikiliza maelezo mafupi toka kwa Mratibu wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Kanali Sambulo Ndrovu(hayupo pichani) kabla ya kufunga rasmi Mafunzo hayo leo Oktoba 02, 2014. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(wa pili kulia) ni Mratibu Msaidizi wa Mafunzo hayo Kamishna Msaidizi wa Magereza toka Nchini Zimbabwe, Didmas Chimvura(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo.



 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi ya ufungaji wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani ambayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo jumla ya Maafisa Magereza 27 toka Nchi za SADC ikiwemo Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Mauritius, Swaziland na Zimbabwe wameshiriki kikamilifu Mafunzo hayo.



 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akikabidhi cheti kwa Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Nchini Tanzania, Pendo Kazumba. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili na yameendeshwa na Kituo cha Mafunzo cha SADC kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza Tanzania(kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC Bregedia Jenerali Christopher Chellah.


 Wakufunzi wa Mafunzo hayo wakisikiliza hotuba fupi ya ufungaji wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC. Jumla ya Wahitimu 27 toka Nchi za SADC wameshiriki Mafunzo hayo kikamilifu katika Chuo cha Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro(wa kwanza kulia) ni Mratibu wa Mafunzo hayo, Kanali Sambulo Ndlovu toka Zimbabwe(wa pili kulia) ni Mkufunzi toka Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Charles Novart(wa tatu kushoto) ni Mkufunzi toka Tanzania, Ahmad Mwidadi(wa pili kulia) ni Mkufunzi toka Zambia, Mrakibu wa Polisi Nchini Zambia, Edward Njovu.


 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari toka Vyombo vya TBC1 na ITV Mkoani Kilimanjaro mara tu baada ya kufunga rasmi Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC leo Oktoba 2, 2014 Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro.


 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa sita kushoto) na Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Magereza Wanawake toka Nchi za SADC ambao wameshiriki kikamilifu Mafunzo ya wiki mbili ya Ulinzi wa Amani katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro.


 Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(kushoto) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(kulia) mara tu baada ya kufunga rasmi Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC(katikati) ni Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo hayo toka Nchini Tanzania, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza, Pendo Kazumba.


Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Magereza toka Nchi za SADC(waliosimama) walioshiriki Mafunzo ya Ulinzi wa Amani ambayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro. Mafunzo hayo yamefungwa leo na Kamishna Jenerali wa Magereza ambapo jumla ya Maafisa Magereza 27 toka Nchi za SADC ikiwemo Tanzania, Mauritius, Afrika Kusini, Swaziland, Botswana, Namibian na  Zimbabwe wamehitimu Mafunzo hayo Maalum ya Ulinzi wa Amani(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).